Siku kadhaa baada ya Naibu waziri
wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Makete Mh. Dkt Binilith Mahenge kutembelea
wilaya ya Makete, wananchi wametoa ushauri wao kuhusiana na suala la barabara
na umeme kama alivyozungumza na wananchi wa
jimbo lake
Wakizungumza na Kitulo Fm baadhi
ya wananchi hao wamesema wamefurahishwa na kauli hiyo ya Mh. Naibu waziri na
kusema anatakiwa kuhakikisha inatekelezwa kwa wakati
Mkazi mmoja wa Makete
aliyejitambulisha kwa jina la Andrea Sanga ambaye pia ni mfanyabiashara amesema
amepokea vizuri kauli ya Mh. Naibu waziri na kuwataka wananchi kuwa na subira
wakati huu wa kutekelezeka wa kauli aliyoitoa
Kwa upande wake Osia Mpandila
amesema kauli hiyo ilimfurahisha na anaamini imewafurahisha wananchi wengi
ikiwemo suala la upelekaji umeme katika eneo la Tandala ambao hatua zitaanza
kuchukuliwa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu
Mei 21 mwaka huu Naibu waziri wa
Maji ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Makete alifanya ziara katika jimbo lake ambapo
pamoja na mambo mengine alizungumzia suala la umeme na barabara katika jimbo
lake