ACHENI KUANZISHA MOTO KICHAA NI HATARI KWA MAZINGIRA

Wananchi wa kijiji cha Mang’oto katika kata ya Mang’oto wilayani Makete wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuchoma mashamba moto bila vibali kwani uchomaji huo wa kiholela unapelekea kuharibu mazingira

Hayo yamezungumzwa na mtendaji wa kijiji cha iwawa bw, Msigwa alipokuwa akizungumza na MTANDAO HUU na kusema kuwa kuna baadhi ya watu wanachoma moto mashamba yao bila kibali na huwa hawawi makini, kwani moto huo wakati mwingine unafika katika kuunguza uoto wa asili na kupelekea uharibifu wamazingira

Amesema wananchi wanatakiwa kuchukua kibali kutoka serikali ya kijiji kitakacho wawezesha kuchoma mashamba yao moto ili endapo kutatokea uzembe katika uchomaji huo na uharibifu wa mazingira kutokea basi itakuwa rahisi kumpata na kumchukulia hatua za kisheria

Aidha bw Msigwa amesema kwasasa inakuwa vigumu kuwakamata watu wanaotorosha moto kwa kuwa watu hawachukui vibali hivyo  ofisi yake imepanga kudhibiti vitendo vya uchomaji moto kwa kuchukua hatua kali za kisheria 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo