Shirika
lisilo la kiserikali la Tunajali linalojihusisha na utoaji wa huduma kwa watu
wanaoishi na vvu wilayani makete limepongezwa kwa kuhakikisha kila kijiji cha
wilaya kina pata elimu ya kuhusu vvu na dawa za kupunguza makali ya virusi
hivyo
Akitoa
pongezi hizo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya makete bw, Daniel Okoka amesema
amefurahishwa na kazi zinazofanywa na shirika hilo la tunajali kwani wamefanikiwa kutoa
elimu kwa vijiji vtote wilayani makete
Amesema
wananchi wanatakiwa kuzitumia dawa hizo za kupunguza makali ya vvu kwani dawa
ya kuuponya kabisa ugonjwa huo haija patikana na kuwaasa wasio na maambukizi
kujikinga na kuwa waaminifu katika mahusiano yao
Aidha
ameyaomba mashirika mengine kuiga mfano wa shirika la tunajali ili kuweza
kupunguza maambukizi ya vvu wilayani makete na kuwataka pia wananchi
kujihusisha na shughuli za kimaendeleo vijijini mwao kwani kwa kufanya hivyo
kutawasaidia kuondokana na umasikini na kuweza kuinua kipato cha familia na
wilaya
Na: Obeth Ngajilo