Wananchi wilayani Makete wameshauriwa kutopuuza maagizo yanayotolewa na madaktari wa mifugo kuhusu kupeleka mifugo yao kupatiwa chanjo na matibabu
Hayo yamezungumzwa na Daktari wa mifugo wilaya ya Makete Nuru Issae wakati akizungumza na wanahabari na kusema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa hawapeleki sehemu itolewapo chanjo au matibabu
Ameongeza kuwa kutopeleka mifugo kupatiwa matibabu ama chanjo kunapelekea wafugaji kutopata mazao mazuri yatokanayo na mifugo yao ikiwemo maziwa, mbolea na nyama iliyo bora
Miongoni mwa magonjwa hayo ni ugonjwa wa ndiganakali ambao mara nyingi huwaathiri ngómbe, ambapo dalili za ugonjwa huo ni pamoja mnyama kupumua kwa shida na kupelekea kifo
Na Anitha Sanga