Viongozi wa serikali ya kijiji cha Isapulano wilayani Makete wamepongezwa kwa kutoa ushirikiano mzuri wakati wa ukaguzi wa usafi wa mazingira katika nyumba za wananchi wa kijiji hicho katika mitaa yote iliyopo kwenye kijiji hicho
Pongezi hizo zimetolewa na maafisa maendeleo wa kata ya Isapulano ambao walikuwa wasimamizi wa zoezi hilo la usafi wakati wakizungumza na wanahabari
Mmoja wa maafisa hao aliyejitambulisha kwa jina la Denis Sinene amesema viongozi wa serikali ya kijiji hicho wametoa ushirikiano wa kutosha katika zoezi hilo
Ameongeza kuwa faini ndogondogo zimetolewana wananchi walioonesha uzembe kwa kutosafisha mazingira yao, wale wasio na vyoo pamoja na wenye vyoo vibovu na agizo kutolewa kwa wale wasio na vyoo kuchimba vyoo ndani ya siku 14 na ofisi yao itafuatilia utekelezaji wa zoezi hilo
Amewataka wananchi wa wilaya ya Makete kuwa na desturi ya kufanya usafi wa mazingira na si kusubiri mpaka ukaguzi ufanyike ili kuepuka kupata magonjwa ya milipuko
Na Obeth Ngajilo