DSM
Ikiwa imesalia miaka mitatu kabla ya mwaka 2015 ambapo nchi zinapaswa kufikia malengo ya milenia ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na vile vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano tathmini ya madaktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi inaonesha kuwa kasi ya Tanzania katika kufikia malengo hayo si ya kuridhisha
Madaktari hao bingwa wa masuala ya uzazi wametoa tathmini hiyo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa mwaka wa madaktari bingwa wa uzazi na magonjwa ya wanawake AGOTA
Akifungua mkutano huo rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhadji Ali Hassan Mwinyi pamoja na kuwapongeza madaktari hao kwa kazi nzuri amekiri kuwepo kwa changamoto katika kuboresha huduma za afya hapa nchini
Kauli mbiu ya mkutano huo ni vifo vya mama na magonjwa ya mtoto tunapofikia miaka 50 ya uhuru je tuko wapi?