Makete
Wazazi na walezi wilayani Makete wametakiwa kuwapeleka watoto wao kwa wingi ili wapatiwe chanjo za magonjwa mbalimbali kwani kwa kutofanya hivyo ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Zainab Kwikwega ameyasema hayo wakati akizindua wiki ya chanjo kiwilaya zoezi lililofanyika katika hospitali ya wilaya ya Makete
Mh. Kwikwega amesema kutowapeleka watoto kupatiwa chanjo ni kuwakosesha hakia yako ya kimsingi ya kukingwa na magonjwa mbalimbali
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Makete Carlo Makombe amesema kuwa zoezi hilo zoezi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo umbali wa kuvifikia vituo vya afya
Akimshukuru mkuu wa wilaya Bi Ester Ngogo ambaye ni mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto amemshukuru Mkuu huyo wa wilaya kwa utayari wake wa kuzindua kampeni hiyo wilayani hapo
Kauli mbiu ya wiki ya chanjo ni “Mtoto asiyechanjwa ni hatari kwake mwenyewe na wengine mpeleke akapate chanjo”