Kurugenzi ya mawasilianao Ikulu jijini DSM imekanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja la kila siku hapa nchini zinazodai kuwa kumekuwa na mazungumzo baina ya rais Jakaya Kikwete na Waziri mkuu Mizengo Pinda kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri wanaoshinikizwa kujiuzulu kwa madai kuwa utendaji kazi wao hauridhishi
Taarifa hiyo imesema rais Kikwete hajaonana wala kufanya mazungumzo yeyote na waziri mkuu Pinda kuhusiana na suala hilo na kwamba hivi sasa Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka bungeni mjini Dodoma
Kwa mujibu wa taarifa hiyo habari iliyochapishwa katika gazeti hilo zinazodai kuwa rais Kikwete anawalinda baadhi ya mawaziri hao ambao wanataka kujiuzulu haina ukweli wowote na ni upotoshaji
Taarifa hiyo imewataka wananchi kutoamini habari hiyo na kutaka wanahabari kuzingatia weledi wanapofanya kazi zao
Wakati huo huo rais Jakaya Kikwete yupo mjini Blantaya Malawi kwa ajili ya kuhudhuria maziko ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Marehemu Prof. Bingu wa Mutharika aliyefariki April 5 Mwaka huu kwa baada ya kuugua ugonjwa wa moyo
Rais Kikwete ni miongoni mwa viongozi wakuu 7 kutoka nchi jirani na Malawi walioshiriki maziko hayo