HABARI ZA WAKATI HUU WADAU, KUMEKUWA NA TABIA MBAYA YA BAADHI YA WATU KUANDIKA TAARIFA AMBAZO SI ZAKWELI NA WAKATI MWINGINE HAWANA UHAKIKA NAZO HASA KUHUSU KIFO CHA STEVEN KANUMBA
KWA MUJIBU WA KAMANDA KENYELA, SI KWELI KWAMBA LULU KAKANUSHA KUHUSIKA NA KIFO CHA KANUMBA KWANI LULU YUKO CHINI YA ULINZI WA POLISI HIVYO HAKUNA MWANDISHI YEYOTE WA HABARI AMBAYE AMEZUNGUMZA NAYE, NA MAZUNGUMZO HAYO YATABAKI MIKONONI MWA POLISI KAMA USHAHIDI NA MUDA UKIFIKA YATATOLEWA NA JESHI HILO AU MAHAKAMA
NA PIA KILICHOMUUA KANUMBA BADO HAKIJAJULIKANA KWANI MWILI WA MAREHEMU HII LEO NDIO UNAFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA NA MADKTARI NA JIBU RASMI LA UCHUNGUZI HUO LITATUMIKA KAMA USHAHIDI KATIKA KESI HIYO
