Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
MKUU wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro, ameiagiza ofisi ya Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,kuchunguza na hatimaye kumkamata mtu anaiyedaiwa kughushi barua kutoka ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI), ikiagiza kutenguliwa kwa zuio la uuzaji wa kahawa mbichi mkoani hapa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kandoro alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi za TAMISEMI barua hizo za vitisho zilizosambazwa katika ofisi yake na wakuu wa wilaya nne za Ileje, Mbeya Vijijini, Mbozi na Rungwe ni ya kughushi hivyo walioisambazwa wanapaswa kukamatwa.
“Hili ni kosa kubwa kwa mtu kuibuka na kutoa vitisho kwa kutumia majina ya viongozi wa juu na ofisi zao, kwani tumefanya uchunguzi wa barua hizo kwanza hazijafuata taratibu za serikali, lakini pia wahusika waliotajwa kutoa barua hiyo toka TAMISEMI wamekataa kuhusika tena kwa maandishi.” Alisema Kandoro.
Alitumia fursa hiyo kuonyesha na kugawa nakala za barua hiyo kwa waandishi wa habari, yenye kumbukumbu namba CAB.65/223/01/23 iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa TAMISEMI M.A Pawaga, ikiwa na baadhi ya maneno yanayosomeka . … “Kama ulivyoitilia mashaka barua hiyo na tathmini iliyofanywa ofisi hii hasa kwa kuzingatia saini ya mwandishi pamoja na mtiririko wa maudhui ya barua hii, tumegundua kuwa ni ya kughushi ,” ilifafanua sehemu ya barua hiyo
Akifafanua zaidi kuhusu zhilo Kandoro alisema hakuna sehemu wala kipengele kwenye sheria ya kahawa kinachozungumzia biashara ya kahawa mbichi, hivyo kitendo cha watu kutaka kulazimisha biashara hiyo ni makosa kisheria.
Hata hivyo Kandoro alipobanwa aeleze uchgunguzi wa awali umebaini mhusika aliyeandika barua hiyo, alisema suala hilo ni la kitaalamu na tayari rimeshafikishwa polisi wao ndio wanauwezo wa kumbaini mhusika na hatimaye kumkamata.
Wakati mkuu wa mkoa akitoa agizo hilo, kanda wa polisi mkoani hapa Advocate Nyombi alipoulizwa hatua zilizofikiwa alidai yuko likizo, lakini baadhi ya maofisa wa jeshi hilo ambao si wasemaji walilihaskikishia gazeti hili kuwa suala hilo lipo mikononi mwa polisi na linafanyiwa kazi
.
Hata hivyo hawakuwa tayari kueleza kama mhusika amekamatwa na kuwataka waandishi kuwa na subira ili uchunguzi ukamilike na hatua zitakazokuwa zimechukuliwa juu ya sakata hilo la kughushi nyaraka muhimu za serikali .
Sakata la ununuzi wa Kahawa mbichi wilayani Mbozi limekuwa la muda mrefu ambapo baadhi ya kampuni zilizopigwa marufuku na serikali ya mkoa kulalamika kuwa uamuzi huo ni wa kibabe kwa kuwa wao wananyaraka halali za serikali zinazowaruhusu kununua kahawa hiyo.
Miongoni mwa kampuni hizo ni Lima ltd , ambayo inadaiwa kughushi barua yenye kumbukumbu namba A.1 80/361/12/09,inayodaiwa kuandikwa na mmoja wa maofisa waandamizi kutoka ofisi ya Waziri mkuu aliyetajwa kwa jina la D. Bandisa,ikimtaka Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya ya Mbozi kuiruhusu kampuni hiyo kuendelea na ununuzi wa kahawa mbichiwilayani humo.
Lakini miaka miwili iliyoipita madiwani kutoka halmashauri zote zinazolima zao hilo zilipinga uuzaji wa kahawa mbichi kupitia vikao vya baraza la madiwani.
Mwenge kuwashwa Mei 11 Mbeya
Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
ZAIDI YA shilingi milioni 170/ zinatarajiwa kutumika na mkoa wa Mbeya katika shughukim za kuzindua mbio za mwenge Mwezi Mei 11 mwaka huu katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jiji hapa
.
Taarifa hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandorio wakati akizungungumza na waandishi wa vyombo mbambali vya habari mkutano huo ulifanyika katika ofisi za mkoa huo jiji Mbeya
Aidha Kandoro alisema kuwa fedha hizo ni zile zilizxo takiwa kutmuika mwaka jana wakati mkoa ulipo pewa jukuma la kuanda shughuli za uwashaji mwenge na baadaye waliwashia mkoani Mara katika kijiji cha Butiama alikozaliwa Baba wa Taifa Mw Juliasi Nyerere.
Aliosema kutokana na kustishwa kwa shughuli hizo mwaka jana serkari imeamua kurtoa fursa hiyo tena kwa mwaka huu kwa mkoa wa Mbeya.
Akifafanua zaidi Kandoro alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili ya watoto wa halaiki,mbalimbali vya habari, matangazo kwa ajili ya uhamasishaji kwa wanachi ilim kujitokeza katika shughuli nzima ya kuwasha mwenge.
Aidha aliongeza kuwa katika fedha hizo hum,la ya shilingi milioni 6 zitatumika kwa ajili ya walimu wano fundisha watioto wa halaiki.
Mkuu huyo wa Mmkoa alibainisha kuwa mwemngi huo utawasha Mei 11 na kukimbizwa katika wilaya zote 8 za mmkoa wa Mbeya ikiepo wilya mpya ya Momba na utakabidhiwa baada ya hapo ataukabidhi mkoa wa Iringa Mei 15 mwaka huu.
Sanjali na hili Mkuu huyo alitoa kauli mbiu ya mbio za mwenge mwaka huu kuwa ‘Sensa ni msingi wa maendeleo yetu’
‘Wito wangu kwa wakazi wa jiji la mbeya na mkoa kwa ujumla ni kujtokeza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki shughuli nzima za uwashaji wa Mwenge mkoani kwetu’ Alisema Kandoro
|
RC AAGIZA MTU ALIYEGUSHI BARUA KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU AKAMATWE
By
Unknown
at
Thursday, April 26, 2012