Na Kenneth Ngelesi, Mbeya

MWENYEKITI wa chama cha mpira wa miguu jiji Mbeya (MUFA) Seleman Haroub  amesema kuwa kuina kilasababu kwa  wadau na washibiki wa timu  za Tanzania Prisons na Mbeya City kuungana na kuisaiodia timu ya Tanzania Prisons kwa kuwa ndiyo timu pekee mkoani hapa iliwakilisha mkoa katika liga kuu msimu ujao.

Kauli hiyo aliitoa juzieneo la Oil com Uyole  wakati wa mapokezi ya timu Tanzania Prisons ikitokea Mkoani Morogoro ilikokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza hatua ya tisa boa na kufanikiwa kutinga ligi kuu baada ya kusota kwa takribani miaka minne maandamano ambayo yaliuteka jiji la Mbeya kwaa maanadamano ya magari na msururu wa watu. .

Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha kuuzia mafuta cha Oli Come Uyole na kuishia katika chuo cha Magereza Ruanda kbala ya hapo timu pamoja baadhi ya vingozi wa Mufa na timu hiyo walipata chakula cha mchana na wachezaji katika ukumbu wa Airport Pab.


Alisema kuwa wao kama chama wanaupokea ushindi  wa Prisons kwa mikono miwili na kwamba wanambea wanatakiwa kutoa mchango wa hali na mali kwa kuisadia timu hiyo na ikiwezekana wapandishe timu nyingine ili kuwe na ushundani.

Alisema kuwa wao kama chama walipenda kupandisha timu zote mbili na ndiyo ulikuwa makati wao kuhakikisha timu zote za Mbeya City na Prisons ziingie ligi kuu lakini timu moja imefanikiwa kuingia ligi kuu kwa hiyo kama wana Mbeya hawana budi kuisasidia timu hiyo na kkujipanga kuipandisha Mbeya Cirty kwa msimu wa mwakani

Hata hivyo mwenyekiti huo aalitmumia fusa hiyo kuwa haasa wachezaji pamoja na viongozi wea Mbeya Cirty kutokata tamaa kwani hata Prisons mwaka jana walishindwa kuingia ligi kuu lakini kwa kuwa hawakukata tamaa wamefanikiwa kuingia.

'Ningependa kuwaasa washabiki,Vviongo, na wachezaji wa timu ya Mbeya City kuto kakata tamaa kwani hata katika hatua wwenzao wa Prisona pale  mkoani Tanga mwaka jana  walishindwa kuingia ligi kuu lakini wamevumilia na kufanikiwa kuingia ligi kuu' alisemna Haroub

Mkoa wa Mbeya katika ligi daraja la kwanza mwaka huu uliwakilishwa na timu mbili ambazo ni Tanzania Prisons na Mbeya City timu iliyomnekana kuwa na washabiki wengi wengi na kuwa na imani nayo lakini wameshindwa kuingia ligi kuu.

Naye kiongozi wa msafara wa timu ya Tanzania Prisons Ernest alisema kuwa ni jambo la kujivunia kwa mmkoa kuwa na timu ya ligi kuu kwan i kwa zaidi ya miaka minne mkoa wa Mbeya umekosa kuona michezo ya ligi kuu licha ya kuwa na vijana wenye vipaji vya kusakata kabumbu.

Aliosema kuwa washabiki kuwa watambue wazi kwamba timu ya Prisons ni yawana Mbeya licha ya kuwa inamilikwa na jeshi la magereza na alipongeza kwa chama mpira wa miguu kwa kufanya mapokezi kwa timu yake.