MAFUA: NI DALILI YA UPUNGUFU WA VITAMIN D


MAFUA ni miongoni mwa magonjwa madogo ya kuambukiza yanayompata karibu kila mtu, kuna wengine huugua zaidi ya mara tatu kwa mwaka na wengine huugua angalau mara moja kwa mwaka, kwa ujumla wake kila mtu huugua mafua na kusababisha usumbufu mkubwa kwa mgonjwa kiasi cha wengine kushindwa hata kufanyakazi.

Kwa mujibu wa utafiti uliokwisha fanyika kuhusu ugonjwa wa mafua, kuna uhusiano mkubwa wa upungufu wa Vitamin D mwilini na ugonjwa huu. Hii ina maana kuwa kiwango cha Vitamin D kinaposhuka mwilini ni rahisi sana mtu kupatwa na mafua na kwamba kushuka kwa kinga ya mwili kwa ujumla kunachangia pia mtu kupatwa na mafua.

Kama ujuavyo, ugonjwa huu hutokea zaidi majira ya baridi au mvua ambapo mwanga wa jua huwa nadra sana. Kama ujuavyo chanzo kikuu cha vitamin D mwilini ni mwanga wa jua (Sunshine).

Kwa maana hiyo, njia pekee unayoweza kuitumia kujikinga na ugonjwa wa mafua ni kuhakikisha unapata mwanga wa jua wa kutosha kipindi cha jua au kula vidonge lishe vya kuongeza Vitamin D kwa muda wa siku tatu ili kuupa mwili kinga hiyo nyakati za baridi panapozuka tatizo hili.

Kwa mujibu wa Dk Cannell kutoka baraza linalojihusisha na Vitamin D nchini Marekani (Vitamin D Council), watu wengi hufanya makosa kwa kudhani kuwa ugonjwa wa mafua huambukizwa na ‘bacteria’ wakati ukweli ni kwamba wanaoambukiza mafua ni Virusi (Viruses), hivyo unapojaribu kujitibu mafua kwa kula ‘anti biotic’ huwezi kupona na mbaya zaidi utakuwa unaendelea kudhoofisha kinga yako ya mwili kwa kuua ‘bacteria’ wote mwilini, wakiwemo wale wazuri.

Kwa kifupi, magonjwa kama mafua huwa ni dalili ya kushuka kwa kinga ya mwili ambako kunaweza kuchangiwa na sababu mbalimbali, kama vile ulaji mwingi wa sukari hasa ‘fructose’ na kula kiasi kingi cha vyakula vitokanavyo na nafaka zilizokobolewa, pamoja na ukosefu wa mazoezi ya mwili ya mara kwa mara.

Mwili unapokuwa na kinga imara, virusi vyovyote vibaya vinapojaribu kuingia mwilini hushindwa kufanya hivyo kwa kukutana na kinga ya asili.

Mazoezi ni sehemu muhimu ya maisha yetu katika kuimarisha kinga ya mwili. Hakikisha unafanya mazoezi mara kwa mara hata kama uko ‘busy’ kiasi gani, lakini tenga muda kwani mbali ya kuimarisha kinga ya mwili, lakini pia huimarisha kiwango cha sukari mwilini hivyo kukuepusha na magonjwa ya kisukari na moyo ambayo mara nyingi huchangiwa na hali ya mwili kukosa mazoezi.
Source: Uwazi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo