KILICHOMUUA KANUMBA HIKI HAPA!!

Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la
...
mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu
kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu
zimeeleza.
 
Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada
ya jopo la madaktari bingwa watano wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia
uchunguzi mwili wa marehemu huyo,
zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya
mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.
 
Mmoja wa madaktari hao ambaye
aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema
waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia
uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.
 
“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa
marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa
6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu
alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa
kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari
huyo.
 
Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumowa upumuaji (cardio-respiratory failure)
“Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo,
ambao endapo unatokea katika sehemu ya
nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa
haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma,
husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji
na hilo limeonekana katika mwili wake.
 
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu,
mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana
tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi
ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia
damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo
ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
 
“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza
kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma
kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa
kwa Kanumba kabla hajafariki.”
 
Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi
huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe
alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa
umevimba na kushuka karibu na uti wa
mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa
upumuaji.
 
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya
machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa
Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo
kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo