Hapa kikao kikiendelea Dosmeza Hotel
Aldo Sanga(kushoto) wa Kitulo Fm akiwa na Shaaban Lupimo wa Uplands FM
Neema Mwanga (kushoto) kutoka Best Fm Ludewa akiwa na Magreth Lupembe
Aldo Sanga akiandika kumbukumbu za kikao hicho
Huyu amaa alinivutia kupiga naye picha
Baada ya kikao
Friday Simbaya kutoka Nipashe naye alikuwepo
Edwin Moshi kutoka Kitulo Fm
Waandishi wa habari mkoa mpya wa Njombe wamelalamikia kitendo cha taarifa za upotoshaji mchakato wa kuanzisha chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe (Njombe Press Club) zilizotolewa na moja ya mwandishi maarufu mkoani humo ambaye jina linahifadhiwa kuwa kikao kilichokuwa kimepangwa kufanywa na wanahabari hao hakipo
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya waandishi hao wamesema mahudhurio finyu ya waliohudhria kikao hicho yamesababishwa na taarifa zilizotolewa na mwandishi huyo kwakuwapigia simu waandishi wengi kuwa kikao hicho kimeahirishwa kumbe si kweli
Kikao hicho ambacho kilifanyika kwenye ukumbi wa Dosmeza hotel kilijadili mambo mbalimbali kuhusu mchakato wa kuanzisha Njombe Press Club
Kikao kijacho kimepangwa kufanyika Jumamosi 14.04.2012 kuanzia saa nne asubuhi katika ukumbi wa Dosmeza Hoteli Mkoani Njombe ambapo viongozi mbalimbali wa Iringa Pres Club wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho
Waandishi kutoka Uplands Fm, Best Fm, Kitulo FM, Nipashe na wengine kutoka Njombe walihudhuria kikao hicho