MAKETE
Wakazi wa kata ya Kiguru tarafa ya Magoma wilayani Makete wamemuomba mganga mkuu wa wilaya ya Makete kuwapelekea muuguzi wa afya aliyepangiwa kufanya kazi kijijini hapo kwa ajili ya kutoa huduma za kiafya
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii Diwani wa kaya ya Kiguru Mh. Simion Mwaikenda ameshangazwa na hatua ya kutopelekewa muuguzi huyo wa afya mpaka sasa kwani kijiji hicho kipo tayari kumuandalia makazi mazuri
Nao wananchi wa kata hiyo wamelalamikia adha wanayoipata kwa kukosa huduma ya afya kijijini kwao
Naye kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Makete Dkt Ahmad Shaaban amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuahidi kwenda kukagua nyumba atakayoishi mhudumu huyo ambayo imeandaliwa na wanakijiji hao, na endapo itakidhi viwango stahili atampeleka muuguzi huyo pamoja na madawa
Na Veronica Mtauka