Watu watano wameuwawa KENYA

Watu watano wameuwawa na wengi kujeruhiwa kwenye shambulio katika kituo cha basi mjini Nairobi, Kenya.

Polisi wanalinda maduka mjini nairobi
 
Inaarifiwa kuwa maguruneti kama mane yalirushwa kutoka kwenye gari dhidi ya kituo cha basi mjini Nairobi - kituo cha Machakos Bus Station, ambacho kilikuwa kimejaa wateja.
 
Shambulio hilo limetokea Jumamosi saa mbili usiku.

Hadi sasa inajulikana kuwa watu watano wamekufa, na wengi kujeruhiwa.

Mbunge wa jimbo hilo la Kamukunji, Yusuf Hassan, alisema alihisabu majeruhi 40 walipokuwa wakifikishwa hospitali ya taifa, ya Kenyatta.

Wakuu bado hawakueleza nani alihusika na shambulio hilo; wala kama washambuliaji ni wa ndani au kutoka nje ya nchi.

Bwana Hassan alisema kuna majonzi na masikitiko mjini Nairobi kutokana na maafa hayo, lakini alisema safari za magari kwenye kituo zimeanza tena.

Aliwasifu watu wa Nairobu kuwa shupavu.

Saa hizo za magharibi ni za harakati nyingi kwenye kituo hicho cha mabasi kutoka mikoani, na huwa na wasafiri wengi.

BBC


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo