MAKETE
Wananchi wilayani makete wameshauriwa kuendeleza kwa bidii kilimo cha miti ili kusaidia kutunza mazingira,lakini pia kuwapatia kipato kupitia biashara ya mbao
Hayo yamezungumzwa na waziri wa mali asili na utalii mhe,Ezekiel Maige wakati akizungumza na baadhi ya wananchi na viogozi mbalimbali wa serikali katika ikulu ndogo wilayani makete
Nae mbunge wa makete Dr,Binilith Mahenge amemshukuru mh,Maige kwa ujio wake na kwa ushauri alioutoa kwa wanamakete,ambapo pia alimuomba waziri kuwasaidia baadhi ya changamoto ambazo zinazoikabili hasa za wananchi na watu wa hifadhi za TANAPA