Wananchi wilayani Makete wametakiwa kutunza na kutumia vizuri miundombinu

Wananchi wilayani Makete wametakiwa kutunza na kutumia vizuri miundombinu inayojengwa na serikali katika mazingira wanayoishi.

Akizungumza na Mtandao huu Afisa mtendaji wa kata ya Iwawa Bw Selemani Kiwone amesema kuwa wakazi wa Makete wamekuwa wakiweka vifaa vya ujenzi kwenye mifereji ya kupitishia maji  na kupelekea maji kujaa barabarani na kuwaribu miundombinu hiyo  ambayo imejengwa na serikali kwa gharama kubwa.

Bw Kiwone ametolea mfano vifaa hivyo vya ujenzi kuwa ni mchanga na mawe vinavyokuwa vimemwagwa kwenye mifereji ya kupitishia maji na kusababisha mifereji hiyo kuziba na maji kujaa barabarani.

Aidha amewaonya wananchi hao kuacha mara moja tabia hiyo kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria kwa kukaidi agizo la serikali 

Na Timotheo Swalo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo