Makete
Jeshi la polisi wilayani Makete linamtafuta Frenk Mkoba Sanga (32) mkazi wa Ihanga kata ya Ukwama wilayani Makete kwa tuhuma za mauaji ya Bi Arusha Sanga (30) yaliyotokea March 5 mwaka huu.
Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo mkuu wa jeshi la polisi wilayani Makete Bwana Rashidi Lundilo amesema tukio hilo lilitokea march 5 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni kwa mtuhumiwa Frenk kumpiga marehemu ngumi shingoni na mateke tumboni baada ya kumwaga pombe yake.
Bwana lundilo amewaomba wakazi wa ndani na nje ya Makete kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi watakapo muona mtuhumiwa Frenk Sanga.
Na Riziki na Enester.