Wananchi wilayani Makete ambao ni wateja wa NMB wamelalamikia usumbufu unaowakumba katika kupata huduma za benki ya NMB tawi la Makete wakati mtandao haupo.
Wateja hao wakizungumza na mtandao huu wamesema kukosa huduma za kuweka na kutoa fedha ilipelekea usumbufu kwao pamoja na kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo.
Akizungumzia tatizo hilo , mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo ya NMB tawi la Makete ambaye hakutaka jina lake litajwe redioni amesema hali hiyo inatokana na kukatika kwa mtandao wa Vodacom ambao wanashirikiana katika kutoa huduma za kibenki kwa wateja
Hata hivyo amebainisha huduma hizo zinaendelea kutolewa japo sio kwa ufanisi wa uhakika.
Zuhura&Godson