Wakazi wa kijiji cha Kitivo kata ya Kerenge Korogwe vijijini, wameondokana na tatizo la uhaba wa maji katika eneo hilo kufuatia kuzinduliwa kwa mradi wa maji ambao utahudumia wakazi zaidi ya 1,600 ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya maadhimisho ya wiki ya maji nchini
Akizungumzia uzinduzi wa mradi huo mkuu wa wilaya hiyo Erasto Sima, amewataka wanakijiji hao kutunza miundombinu ya maji ili mradi huo uwe endelevu kwa manufaa ya wakazi wa eneo hilo
Vituo saba vya kuchotea maji kila kimoja kina uwezo wa kuhudumia watu 250
Uzinduzi huo umekwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya maji kama anavyozungumza mkuu wa wilaya hiyo
Nao baadhi ya wananchi wa korogwe waliokuwa wakipata shida ya kukosa maji walishukuru kwa uzinduzi huo kwani unafuu wataupata
WAKATI HUO HUO
Jijini Tanga nako wamezindua maadhimisho ya wiki ya maji
Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka Jamal Ngereja katika wiki hii ya maadhimisho ya wiki ya maji wametoa ofa kwa wateja wao
Amesema wateja waliokatiwa maji muda mrefu pia watatembelewa ili kuangalia namna ya kuweza kuwarejeshea huduma ya maji kwa kufuata taratibu