Naibu waziri wa ujenzi Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye amerejea kazini baada ya kutoka kwenye matibabu nchini India , amesema waandishi wa habari waache kutoa habari kuhusu ugonjwa wake na badala yake taarifa itatolewa na tume iliyoundwa na serikali kwa ajili hiyo
Mh. Dkt Mwakyembe ambaye amezungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili ofisini kwake, amesema ni vema waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla wakasubiri tume iliyoundwa kushughulikia suala lake ifanye kazi yake na kisha kutoa matokeo
"Jamani mimi nina familia mke wangu na watoto wanachanganywa na habari za ugonwa wangu,tume imeundwa na itatoa majibu, mimi nipo hai sijafa na nitaendelea kuishi"alisema Mwakyembe
.jpg)