WANANCHI katika Manispaa ya Morogoro wamelitupia lawama jeshi la polisi mkoani hapa kwa kitendo chao cha kumuachia kijana aliyeonekana kuwa kibaka mzoefu wa simu ambaye baadaye walimwachia baada ya kukamatwa kuiba simu majira ya mchana katika dula la mfanyabiashara mjini Morogoro.
Kijana huyo ambaye alipewa mkong'oto mkali na wananchi aliokolewa na polisi ambaye waliondoka naye pamoja na mmilikiwa duka hilo la simu.
Katika hali ya kushangaza, kijana huyohuyo jioni alimpora simu Mwinyi Kazimoto, mchezaji wa timu ya Simba iliyokuwa ikicheza na timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu.
Kibaka huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana alipora simu hiyo baada ya mechi hiyo.
Hata hivyo mchezaji wa Simba, Uhuru Selemani, alisaidiana na kiongozi wa klabu hiyo,
Geoffrey Nyange, kumfukuza kibaka huyo na kufanikiwa kumkamata na kumwangushia kichapo kwa kusaidiana na mashabiki wa soka waliokuwa uwanjani.
Geoffrey Nyange, kumfukuza kibaka huyo na kufanikiwa kumkamata na kumwangushia kichapo kwa kusaidiana na mashabiki wa soka waliokuwa uwanjani.
Kibaka huyo aliokolewa tena na polisi ambao waliondoka naye.
source:Global publishers