Ally Choki ametangaza kujitoa katika shindano la kuwania Tuzo ya Kill Music

Mkurugenzi na Mwanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki ametangaza kujitoa katika shindano la kuwania Tuzo ya Kill Music kwa kile alichodai haoni faida ya kushiriki.

Choki alisema kujitoa kwake kunatokana na ushiriki wake kila mwaka bila kupata chochote, hivyo haoni haja ya kuendelea kuwa ndani ya shindano hilo kwani limejaa ubabaishaji.

“Tuzo hizi sizipendi kwa sababu siyo za kweli, kila mwaka huwa nashiriki lakini sijaona faida yake, nawaomba Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wazitoe nyimbo zangu zote kwenye shindano hilo,” alisema Choki.

Choki anaungana na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Sykes a.k.a Dully Sykes,ambaye naye alijitoa Wengine ni Tid, hivi karibuni kwa madai kuwa tuzo hizo ni za uongo na hazina maana yoyote kwake..

Na Pro 24


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo