Nikki Mbishi na Stereo kutangaza kujitoa kwenye kundi la LUNDUNO.

March 2 2012 imeingia kwenye kitabu cha kumbukumbu za 2012 baada ya marapa wawili Nikki Mbishi na Stereo kutangaza kujitoa kwenye kundi la LUNDUNO.

Aliyekua wa kwanza kujitoa ni Stereo ambae aliamplfy kwamba “najua hizi taarifa zitashtua watu lakini inabidi wazikubali manake nilijiunga na Lunduno Mwenyewe na hata kujitoa nimejitoa mwenyewe bila kulazimishwa, mambo yamekua mengi mimi nasoma sasa hivi mwaka wa pili chuo cha Ardhi kwa hiyo time inabana, kitu kingine ni kwamba sitaki nibanwe na kazi nikashindwa kutekeleza majukumu ya Lunduno alafu watu waseme naringa, vilevile nataka pia kufanya mambo yangu mwenyewe, sijagombana na mtu yoyote, Nikki na One ni watu ambao nafanya kazi nao M-LAB studios na tutaendelea kuwa kitu kimoja kwa sababu tunafanya kazi kwenye record label moja”

Nikki Mbishi amesema sababu za yeye kujitoa ni kukinzana wenyewe kwa wenyewe, yani imetokea hawaelewani mara kadhaa sasa ili kuendeleza heshima, ni bora kila mtu achukue zake ili heshima iendelee kuwepo.

Hii ishu imetokea baada ya Nikki Mbishi kuandika kwenye page yake ya facebook kuhusu kumtoa kwenye kundi hilo member mwingine ambae ni Suma Mnazaret january 16 mwaka huu.

Na millardayo.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo