Mji wa Makete
MAKETE 22.02.2012
Wafanyabiashara wa soko la wakulima Makete Mjini wametoa kero kubwa wanayoipata pindi wanapohamishwa kila mwisho wa mwezi kwenda kwenye mnada katika soko la Ngiu wilayani hapa
Wakizungumza na Kitulo Fm sokoni hapo wafanyabiashara hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe wamesema wakienda kuuza bidhaa zao katika mnada huo, bidhaa hizo hazinunuliwi kama wanavyotaka hali inayowasababishia kupata hasara
Kutokana na hali hiyo wameiomba serikali kutafuta wafanyabiashara wakubwa ili wanunue bidhaa zao kwa jumla kuliko ilivyo sasa ambapo bidhaa zao huuzwa kwa reja reja
Kwa upande wake Afisa biashara na masokao wilaya ya Makete Bw. Edonia Mahenge ameahidi kuwahamasisha wafanyabiashara kutoka Njombe na Makambako kuja kununua bidhaa za wafanyabiashara wa Makete kwa bei za jumla na rejareja
Hata hivyo amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kupeleka bidhaa zao katika mnada huo, kwani wafanyabiashara mbalimbali kutoka nje ya wilaya ya Makete hununua bidhaa nyingi hali inayowasaidia kutopata hasara