MAKETE 22.02.2012
Wananchi wilayani Makete wameshauriwa kujiwekea mazoea ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Kitulo pamoja na vivutio mbalimbali vya kitalii ikiwemo pori la akiba la mpanga kipengele
Hayo yamezungumzwa na Afisa maliasili wilaya ya Makete Bw. Uhuru Mwembe alipokuwa akizungumza na Kitulo Fm na kuongeza kuwa mwitikio wa wanamakete kutembelea vivutio hivyo bado hauridhishi ukilinganisha na watalii wa nje
Amesema wilaya ya Makete imebahatika kuwa na hifadhi ya Kitulo ambayo ina vivutio kama uwanda wa nyasi, milima pamoja na maporomoko ya maji lakini bado wanamakete hawana utaratibu wa kutembelea maeneo hayo
Aidha Bw. Mwembe amewataka wananchi wa Makete kuanza kujiwekea utaratibu wa kutembelea hifadhi hiyo kwani kwa kufanya hivyo watajifunza mambo mbalimbali ambayo hawayafahamu