Mwanamuziki Jean Pierre Nimbona ‘Kidum’ amesema kuwa anafikiria kujenga uwanja mkubwa wa burudani utakaokuwa na shughuli nyingi nchini Burundi Kidum, aliyasema hayo baada ya kuvutiwa na muundo wa uwanja wa kisasa wa burudani wa Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.
Dar Live ni uwanja wenye vivutio vingi, kama vile michezo ya watoto, jukwaa kubwa la kisasa lenye mfumo bora kabisa wa sauti, taa za kiwango cha juu, huku pia kukiwa na eneo kubwa la burudani, vitu ambavyo vimemgusa Kidum.“Huu ni uwanja mkubwa sana.
Unavutia na kwa kweli ukiwa hapa mwanamuziki anafurahia kutoa shoo,” alisema Kidum.Aliongeza: “Nitajenga Burundi lakini tatizo kule ni amani. Unaweza kuandaa kitu kizuri lakini matokeo yake watu wakavamia na risasi.”...
NA PRO 24DJS