Mwenyekiti wa Chama cha Wanamuziki wa Kizazi Kipya (Tuma), Fredrick Mariki ‘Mkoloni’, amesema kuwa muafaka wa wadau wakubwa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Rugemalila Mutahaba, ni ushindi kwa Vinega wa Anti Virus.
TAARIFA: Tunapenda kupongeza mafanikio yaliyotokana na mixtape ya Anti virus vol 1 na vol 2, kwani ndiyo yaliyopelekea muafaka uliokuwa umetugawa wasanii na kutufanya tukose haki yetu ya msingi kama chombo pekee chenye dhamana ya kupokea misaada kutoka ndani na nje ya nchi hasa ikizingatiwa kuwa T.F.U ni kanjanja iliyokuwa imejificha kwa maslahi ya watu wachache na badala yake sasa kinakwenda kuwa chombo cha wasanii wanachama wa Tuma kwa wale waliopo na watakaoendelea kujisajili......
Kwetu sisi Tuma tunafurahi sana na kupongeza jitihada za makusudi zilizochukuliwa na serikali kupitia wawakilishi wake yaani Dkt Nchimbi na Mh Tundu Lissu kwa kuweza kutambua hoja za Vinega zilikuwa za msingi na hatimaye kufuta T.F.U, lakini pongezi zaidi ni kwa hatua ya kukubali kuirejesha studio iliyotolewa na Rais kwa kuileta kwenye mikono salama kwa maana ya Tuma chini ya Basata.
Tunalipongeza hilo na tunapenda kuwaambia wasanii wengine ambao walituona sisi ni wajinga tusiokuwa na akili kuwa tulijua tunachokisimamia na kimekuwa sasa ni wakati muafaka wa kuunganisha nguvu zetu ili tuendeleze harakati na mapambano ya kumkomboa msanii wa Tanzania kwa kuwachana mameneja masoko, wasambazaji, madj wenye utamaduni wa zamani na yeyote atakayejitokeza na kuzingua tasnia ya sanaa kwa jumla.
Tunasisitiza umoja na kujiamini pasi kuyumbishwa na kwa kuzngatia hili tunapenda watu wajue kuwa vita yoyote lazima iwe na malengo... sasa adui kanyanyua bendera nyeupe juu watu walitaka tumuue????
Na baada ya kumuua vipi madai yetu??? Tulikuwa na ajenda na zote zimesikilizwa na kukubaliwa na si vinginevyo sasa ni kusonga mbele kwa mixtape vol 3 kwa virusi wengine.....ikumbukwe harakati haziwezi kumalizwa kwa kutatua tatizo moja, bado wengine kibao wapo na tuna kazi nao vile vile!
Mkoloni
Mwenyekiti Tuma.