Kundi la muziki wa kizazi kipya la JNY UNIT linaomba support ya kutosha kutoka kwenu ili liweze kusonga mbele kisanii
Kundi hilo ambalo linatamba na NGoma ya Mpweke ambayo wameiachia maalum kwa ajili ya wapendanao yaani valentine day ni moja ya makundi yanayokuja kwa kasi kimuziki hapa nchini
Akiongea na mtandao huu kiongozi wa kundi hilo Deogratius Simon Mongela (King DESAMO) amesema wao wamejipanga vizuri kimuziki hivyo kuwataka mashabiki kuwapa sappot ya kutosha ikiwemo kusikiliza kazi zao wanazozifanya
Mbali na ngoma hiyo ya mpweke wanayotesa nayo sasa pia kundi hilo la JNY UNIT linatesa na wimbo mwingine wa ngoma ya Club