Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Zainab Kwikwega amewataka wfanyabiashara wa kusaga na kukoboa nafaka wilayani Makete kushusha bei za kukoboa na kusaga nafaka kutokana na wao kupandisha zaidi ya asilimia mia moja
mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha baina ya uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Makete na wafanyabiashara hao kukao kilichofanyika kwenye ukumbi wa HIMA Makete
Mkuu hyuo ameongeza kuwa ni wakati wa wafanyabiashara hao kutumia busara katika kupata suluhu ya bei kwani imepanda kutoka sh.700 kwa kukoboa/kusaga debe moja ya nafaka hadi sh.1,500
ameongeza kuwa imekuwa kawaida kwa wafanyabiashara wilayani Makete kuuza mara dufu ya bei ya kawaida ya bidhaa au mara tatu
Kwa upande wao wafanyabiashara hao wamesema kupanda kwa gharama za umeme na maji ni moja ya sababu kubwa inayopelekea wao kupandisha gharama ya kusaga na kukoboa nafaka
Kikao hicho kilichohusisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Makete, Mkurugenzi mtendaji halmashauri wa wilaya ya Makete Imelda Ishuza, Afisa biashara wa wilaya pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara hao, hadi nakwenda mitamboni wamekubaliana bei elekezi iwe kati ya sh. 1000 hadi 1200, na bei hiyo itapelekwa ofisini kwa mkuu wa wilaya kwa maamuzi