Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mashirika ya uma Zito Kabwe amesema kuwa tuhuma za kuuzwa sehemu ya mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira umeishtua kamati yake hivyo watalipeleka kwa kamati ya bunge inayoshughulika na masuala ya nishati na madini
Zito ameyasema hayo wakati akizungumza kupitia kipindi cha Power breakfast kinachorushwa na Clouds Fm na kusema kamati hiyo ya nishati na madini ndiyo yenye mamlaka ya kulijadili swali hilo kwa mujibu wa kanuni za bunge
Pamoja na mambo mengine kamati hiyo ya mashirika ya uma imeagiza kuwa eneo lote la mgodi huo wa kiwira libaki mikononi mwa serikali na si kwa mwekezaji yeyote!