ASKARI POLISI AUAWA NA JAMBAZI

Mtu mmoja anayesadikika kuwa ni jambazi amemuua askari mmoja wa jeshi la polisi kwa risasi pamoja na kumjeruhi kwa risasi afisa upelelezi wilaya ya Arusha mjini wakati askari hao wakiwa kwenye harakati za kumweka chini ya ulinzi mtuhumiwa huyo

Tukio hilo limetokea katika wilaya ya shangari katika wilaya ya Arumeru nnje kidogo wa mji wa Arusha baada ya askari hao kuvamia nyumba moja iliyokuwa imemhifadhi mtuhumiwa huyo wa ujambazi

Mtuhumiwa huyo aliyefahamika kama Pokea Samson ametorokea kusikojulikana baada ya kufanya mauaji hayo kwa kutumia silaha aliyokuwa akiitumia

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Arusha Tobias Andengenye amesema baada ya tukio hilo uchunguzi umefanywa kwnye nyumba nyingine ambayo hutumiwa na kundi la jambazi huyo na wmefanikiwa kukamata risasi kadhaa

Polisi mkoani Arusha wnaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo ma kutamgaza donge nono kwa atakayefanikisha kukamatwa kwake


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo