Mimi nilidhani kuwa uchakachuaji huwa unafanyika katika Mafuta au kura ila sasa imehamia katika suala la madawati ambapo wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Iwawa wilayani Makete kuchakachuliwa!
Hali hiyo imegundulika baada ya madenti hao wenyewe kudai kuwa wao wamepeleka dawati na viti vya plastiki lakini cha ajabu ni kwamba wao wamenyang'anywa na waalimu wao na kupeleka viti hivyo vikaliwe na wanafunzi wa kidato cha tano a.k.a "A" Level.
Sakata hilo ambalo limejitokeza katika shule ya sekondari iwawa limezua mtafaruku wa chini chini ambapo jitihada za kuonana na uongozi wa shule hiyo pamoja na Afisa Elimu Sekondari wilayani Makete bado linaendelea.
NITAZIDI KUKUJULISHA KWA KADRI NITAKAPOPATA HABARI HIZIII