Makete 21.01.2011
Bw. Kawaida Ngigwa (75) mkazi wa kijiji cha Uganga kata ya Bulongwa wilayani Makete amekutwa akiwa amechinjwa nyumbani kwake
Akizungumza na Kitulo Fm ofisini kwake Mkuu wa jeshi la Polisi wilaya ya Makete Bw. Rashidi Lundilo amesema tukio hilo limetokea tarehe 19/01/2011 majira ya asubuhi nyumbani kwa marehemu
Bw. Lundilo amesema kuwa akiwa nyumbani kwake marehemu Kawaida amekutwa ameuwawa kwa kukatwa shingo na silaha yenye ncha kali na watu wasiojulikana
Amesema kuwa baada ya polisi kuuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuchunguza walibaini kuwa mwili wa Bw. Kawaida ulikuwa umetolewa ulimi na kuongeza kuwa kifo chake kinahusishwa na imani za kishirikina
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na linawaomba wakazi wa Uganga kuwa anayefahamu aliye husika na tukio hilo kutoa taarifa kwa jeshi hilo na wao watamlinda kwa kutomtaja.
By Edwin Moshi