Mamia wajitokeza kuuaga mwili wa Le Mutuz

Na Said Mwishehe


NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu pamoja wabunge wengine wa Bunge hilo wamewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa mtoto wa Waziri Mkuu John Malecela, William Malecela aliyefariki dunia Mei 14 mwaka huu.

Waombolezaji hao wameaga mwili wa William maarufu kwa jina la Lemutuz ambaye pia ni mmiliki wa Blogu ya Lemutuz wametoa heshima zao za mwisho na kumuaga wa mwili wake leo Mei 15/anatarajiwa kuzikwa Mei 17, 2023 katika Kijiji cha Mvumi mkoani Dodoma.

Kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa Lemutuzi , ndugu , jamaa na marafiki wametoa salamu za pole huku wengine wakimuelezea kwa nama ambavyo wamemfahamu .

Pamoja na mambo mengine waliopata nafasi ya kumuelezea Lemutuz wamesema alikuwa ni mkweli na mtetezi mkubwa wa Serikali na watu binafsi na aliamini katika ukweli, kwani hakuwa mnafiki.

Akitoa salamu za shukrani kwa waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Lemutuzi, Mzee Samuel Malecela amewashukuru wote ambao wamefika kwa ajili ya kumuaga William(Lemutuz)

"Nina mambo mawili, moja kwa ukoo wa Malecela tunataka tuahidi wote waliosema mema kuhusu William tunayachukua kama nyota ya kutuongoza, kama hatuwezi kufanya hivyo tutakuwa watu wa ajabu...

"Pili nataka niwashukuru wote mliopo hapa, sina cha kuwalipa ila ninamuomba Mwenyezi Mungu awajaalie moyo mwema wa kusaidiana na kukimbiliana kwenye masuala mbalimbali, tunasema ahsanteni sana, " amesema mzee Malecela.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi ya Lemutuz , Omar Kimbau wakati anamkaribisha mzee Malecela ametumia nafasi hiyo kumshukuru mzee kwa kukubali mtoto wake kuagwa na marafiki, ndugu na jamaa zake wa Dar es Salaam.

Pia ametumia nafasi hiyo kwa niaba ya waombolezaji wengine kumpa pole mzee Malecela kwa mitihani anayopitia ya kuondokewa na watoto wake kwani Lemutuz anakuwa mtoto wa nne kufariki ndani ya kipindi kifupi.

Kwa upande wake mmoja wa rafiki wa Lemutuz Juma Pinto ametumia nafasi hiyo kumuelezea Lemutuz ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu kwa mrefu na kwamba anakuwa kati ya marafiki wachache ambaye alikuwa anaweza kumshauri akamsikiliza kwani akimshauri anaweza kumsikiliza.

"Kwangu William alikuwa mtu pekee ambaye nikimwambia jambo ananisikiliza lakini ni mtu ambaye alijitahidi kuwa na connection , nakumbuka wakati Jamii Forum imeanzishwa mimi nilikuwa Uingereza na yeye alikuwa Marekani...

" Hivyo tukawa tunafanya kazi ya kupambana kutetea viongozi wa Serikali pamoja na Serikali pale ilipokuwa inashambuliwa kwenye Jamiiforum , na William alichokifanya kwa wakati huo ndio alikuwa ametuunganisha watu wa nchi tatu Marekani, Uingereza na Japan.

"Mimi niliwahi kurudi nchini na William alirudi baadae na alipokuja akaniambia nimerudi tukakutana na muda wote tumekuwa , hivyo tumekuwa pamoja na hadi umauti na tumekaa naye sana nyumbani kwangu kabla ya mimi kuhama na kumuachia nyumba ambayo ndio amekuwa akiishi hadi anafikwa na umauti, " amesema Pinto.

Kwa upande wake Multaza Mangungu ambaye ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kilwa Kaskazini ameeleza namna alivyomfahamu Lemutuz ambaye amuelezea ni mtu aliyependa kusimama kwenye ukweli na hakukubali kuwa mnafiki.

Baada ya kutolewa na kuaga mwili wa Lemutuz safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ilianza kwa ajili ya kuusafirisha mwili wake kwa ndege ambayo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.
 Waombolezaji wakiwa katika zoezi la kuaga mwili wa William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz ambaye pia ni mmiliki wa Blogu ya Lemutuz katika Viwanja vya Karimjee leo Mei 15,2023 Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda akitoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz ambaye pia ni mmiliki wa Blogu ya Lemutuz katika Viwanja vya Karimjee leo Mei 15,2023 Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz ambaye pia ni mmiliki wa Blogu ya Lemutuz katika Viwanja vya Karimjee leo Mei 15,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela ambaye pia ni baba wa marehemu William Malecelaakizungumza wakati wa zoezi la kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz ambaye pia ni mmiliki wa Blogu ya Lemutuz katika Viwanja vya Karimjee leo Mei 15,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe.John Samuel Malecela ambaye pia ni baba wa marehemu William Malecelaakizungumza wakati wa zoezi la kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz ambaye pia ni mmiliki wa Blogu ya Lemutuz katika Viwanja vya Karimjee leo Mei 15,2023 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo