Babu wa miaka 81 mbaroni kwa kumbaka mtoto wa miaka 11

MKAZI wa kata ya Nyamatare Manispaa ya Musoma mkoani Mara, Katembo Mnubi au Wajanga mwenye umri wa miaka 81 amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Musoma akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11, mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Nyamatare. Ikiwa atakutwa na hatia, anaweza kuhukumiwa kifungo cha kuanzia miaka 30 jela.


Akisoma kesi hiyo mbele ya mwendesha mashitaka wa serikali Beatrice Mgumba, Hakimu wa wilaya ya Musoma Aristeda Tarimo amesema kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 2, 2023 majira ya saa nne za asubuhi kipindi mtoto huyo akiwa katika mapumziko ya vipindi vya darasani.

Tarimo ameiambia mahakama ya Wilaya kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akimtendea unyama mtoto huyo zaidi ya mara moja ambapo siku ya kwanza mtuhumiwa alimwita mtoto huyo akiwa mapumziko ya vipindi vya darasani na kumtaka aende ndani kwakwe akachukue fedha na akamnunulie sigara.

Amesema baada ya mtoto huyo kuingia ndani ndipo mtuhumiwa alipofunga mlango na kukamata kisu ambacho kilikua maeneo ya kitandani na kumuonya kuwa endapo angepiga kelele angelimchoma kisu na baada ya hapo alimvua nguo na yeye pia kuvua nguo na kuanza kumfanyia unyama huo na mwisho kumpa Sh 100.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo