Wananchi walalamika kuchezea Kichapo cha Mtendaji wao

Wananchi wa Kijiji cha Saragulwa wilayani Geita wametaka kuchukuliwa hatua kwa Mtendaji wa kijiji hicho, Wasira Bulegi kwa madai kuwa amekuwa akiwachapa viboko pamoja na kuwalazimisha walipe faini ya mifuko ya saruji pindi wanapokiuka taratibu walizojiwekea katika kijiji hicho.


Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi za Afisa Mtendaji wa kijiji cha Saragulwa.

Akijibu malalamiko hayo mtendaji wa kijiji hicho ambaye ni mlalamikiwa amekiri kumchapa viboko mwananchi mmoja ambaye alibainika kuiba mfugo.

Kufuatia tukio hilo, Magembe amemuonya mtendaji huyo kuacha tabia ya kuwachapa wananchi viboko na badala yake kufikisha mashauri yao katika mamlaka husika pindi wanapokosa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo