Serikali kujenga bweni lililoungua moto Vwawa


Kufuatia tukio la moto uliounguza bweni katika shule ya sekondari ya Vwawa iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe, uongozi wa wilaya hiyo umeahidi kuanza ujenzi wa bweni hilo mara moja.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwapa pole wanafunzi kufuatia tukio hilo lililounguza bweni lililokuwa likitumiwa na wanafunzi zaidi ya 60.

Moto huo umeteketeza kabisa bweni la wanafunzi wa kike na vitu vilivyokuwamo ndani ikiwa ni pamoja na magodoro na vifaa vingine vya wanafunzi.

Hadi sasa chanzo cha moto huo uliotokea leo majira ya asubuhi, bado hakijajulikana. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo