Polisi nchini Nigeria wamemkamata msanii ambaye huvalia mavazi ya kike kwa madai ya kuwahadaa wanaume kumposa.
Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina bandia la Maryam, analotumia kuwahadaa wanaume, anadaiwa kujifanya mwanamke kwenye mitandao ya kijamii. Jambo la kufurahisha ni kwamba 'Maryam', aliwavutia wanaume kadhaa kihisia ambao walikuwa tayari kumuoa bila kujua kuwa yeye ni mwanaume.
Wanaume wengi walianguka kwenye mtego wake na hata kuwekeza kihisia katika uhusiano huo huku wengine wafikia kwenye hatua ya kumposa.
Katika njia ya kumshinikiza awe wao wa maisha, wanaume hao walisemekana kutoa maelfu ya naira kwa Maryam ili kumfanya akubali posa lao. Hata hivyo, tamaa zao zilikatishwa baada ya kugundua kuwa mtu waliyekuwa wakimvizia hakuwa mwanamke bali ni mwanamume mwenzao.
Kufuatia kukamatwa kwake, mtuhumiwa huyo wakati akihojiwa alikiri kutenda kosa hilo na kuongeza kuwa alijipatia fedha nyingi zikiwemo noti za kigeni kutoka kwa wanaume kadhaa waliokuwa wakimtaka kimapenzi.
Kujibu taarifa hizo, chanzo cha polisi kilithibitisha kwamba Maryam amezuiliwa na atakabiliwa na mashtaka.
Chanzo: TUKO.co.ke
