Makachero wa DCI wamemkamata Joseph Muema mwenye umri wa miaka 45 baada ya kumnajisi nyanya mwenye umri wa miaka 77 anayeugua kiakili katika boma lake.
Tukio hilo linalosemekana kuwaacha wakaazi vinyua wazi lilitokea katika kijiji cha Ikuuni eneo bunge la Mwala katika kaunti ya Machakos ambapo mshukiwa alienda mafichoni baada ya kutekeleza unyama huo.
"Maafisa wa upelelezi wa DCI wamemkamata mwanamume aliyembaka nyanya aliyekuwa mgonjwa wa akili jana usiku kabla ya kwenda mafichoni huko Mwala Kaunti ya Machakos. Joseph Muema, 45, kwa sasa yuko rumande kufuatia kukamatwa kwake kwa kitendo alichokifanya cha kuchukiza ambacho kiliwashangaza wakaazi," DCI walisema kupitia katika mtandao wao wa Twitter.
Kulingana na taarifa iliyochapishwa na DCI mshukiwa alijificha na kuingia katika chumba alimokuwa amelala nyanya huyo kabla ya kutekeleza unyama huyo. "Mshukiwa aliingia katika chumba cha kulala cha mwathiriwa mwenye umri wa miaka 77 kabla ya kunaswa na mwanawe mwathiriwa ambaye alikuwa ameenda kumjulia hali mamake mwendo wa saa 11 jioni," Makachero wa upelelezi walisema.
Muema pamoja na muathiriwa walipelekwa katika kituo cha matibabu cha Mbiuni ambapo matokeo ya uchunguzi yalithibitisha kuwa muathiriwa likuwa amenajisiwa. "Mshukiwa na mwathiriwa walipelekwa katika hospitali ya Mbiuni ambapo vipimo vya afya vilithibitisha kuwa mwathiriwa alibakwa," taarifa ya DCI ilidokeza.
Kwa sasa Muema amezuiliwa na maafisa wa usalama akisubiri kufunguliwa mashtaka kwa kosa la ubakaji.