Mama ajifungua ndani ya boti Zanzibar kwenda Dar

 


Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Maryam Yahya Maulid mwenye umri wa miaka 25, Aprili 14, 2023 saa 7:45 mchana amejifungua mtoto wa kiume akiwa ndani ya Boti ya MV Kilimanjaro V iliyokuwa ikitokea Zanzibar kwenda Dar es Salaam.


Mwanamke huyo amejifungua salama kwa msaada wa Daktari Suleiman wa Sealink na mtoto huyo amezaliwa na uzito wa kilogramu 2.5 na kupewa jina la Kilimanjaro V.

Akizungumza na Azam Online, mume wa mwanamke huyo, Isaka Musa amesema kwasasa mama na kichanga chake wanaendelea vizuri na wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Temeke kwaajili ya uchunguzi zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo