Bibi wa Miaka 78 Akamatwa kwa Kuingia na Kupora Benki kwa Mara ya Tatu


Bibi mwenye umri wa miaka 78 ambaye amewahi kuwa na hatia mbili za kuiba benki ametiwa mbaroni tena kwa wizi huko Missouri, Marekani polisi wamesema. 


BiGooch Bonnie aliingia katika Benki ya Kifedha ya Goppert na kudaiwa kukabidhi barua kwa mtoa pesa akidai maelfu ya pesa taslimu. Pia aliacha barua inayosema "Asante samahani sikukusudia kukutisha" kabla ya kuondoka na pesa taslimu. BiGooch anazuiliwa korokoroni huku akitakiwa kulipa bondi ya kiasi cha $25,000 sawa na KSh3.3m.


Kulingana na Kansas City Star barua za korti zilisema alifika benki akiwa amejifunika uso kwa barakoa, miwani nyeusi na glavu Jumatano iliyopita na kumshurutisha mhudumu kumpa 13,000. Baada ya kitendo hicho waendesha mashtaka walisema, aliondoka na gari lake. 


Polisi wa Pleasant Hill Missouri waliitikia wito na walimfuata na kumkuta bikizee huyo ndani ya gari lake akiwa mlevi, huku pesa zimetapakaa. BiGooch alitiwa mbaroni na kushtakiwa kwa kosa la kupora au kujaribu kuiba kutoka kwa taasisi ya kifedha. 


"Maafisa walipomkaribia walichanganyikiwa walipoona ni nyanya" kamanda wa Pleasant Police Hill Tommy Wright alinukuliwa na Kansas City Star. Aliongeza: "Hatukuwa na uhakika hapo awali kwamba tulikuwa tumemkamata mshukiwa sahihi." BiGooch amewahi tena kukamatwa kwa wizi huko California mnamo 1977, pia wizi wa benki mnamo 2020. 

Muda wake nje ya jela lakini chini ya jicho la serikali 2020 uliisha mnamo Novemba 2021. Wright alisema BiGooch hana maradhi "yanayotambuliwa", lakini kwa sababu ya umri wake, idara ilikuwa ikijaribu kubaini ikiwa sababu zozote za kiafya zingeweza kuchangia tukio hilo. 

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo