Wanaodaiwa kuteka magari Njombe wakamatwa baada ya kudhulumiana

Watuhumiwa 17 wa matukio ya utekaji wa magari na uporaji wa fedha na mali kwa kutumia silaha mkoani Njombe wamekamatwa baada ya kufanyika msako mkali uliohusisha Makamanda kutoka mikoa ya Njombe, Ruvuma, Songwe, Iringa na Mbeya.


Sambamba na kuwanasa watuhumiwa wa ujambazi wanaohusika na utekaji wa magari katika msako huo,vikosi vya polisi vimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine 70 wanaodaiwa kuhusika na matukio ya wizi na uvunjaji majumbani ambapo katika uchunguzi wa awali imeonekana wengi wao wanatoka mikoa mingine kuja kufanya kazi kwenye makampuni ya wachina ya ujenzi wa barabara.

Akitoa taarifa ya matokeo ya operesheni iliyofanyika katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja na vikosi vya polisi wa mikoa hiyo,Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema katika kundi hilo la wa tuhumiwa wa ujambazi wapatao 17 kuna wanawake watatu waliokuwa wakishirikiana nao kuweka mipango huku Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga akisema katika uchunguzi wa awali wamebaini ongezeko la matukio ya kihalifu mkoani Njombe umetokana na uwepo wa fursa nyingi za uchumi.

"Tulibaini kuwa wageni ndio waliokuja kufanya uhalifu na walikuja kufanya kazi katika kambi ya wachina na kuna mwenyeji alikuwa amewahifadhi sasa kulikuwa na hali ya kutoelewana baada ya vitu vilivyoibiwa kuviweka sehemu tofauti, Hawa wahalifu 17 waliokamatwa wengi wao ni waliokuja kuomba kazi za udereva lakini kazi zinapochelewa wanaamua kufanya kazi nyingine" amesema Hamis Issah Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe

Makamanda wamesema imekuwa jambo rahisi kuwanasa watuhumiwa kwasababu baada ya kutekeleza matukio ya uhalifu walizurumiana fedha na kuanza kugombana.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo