Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe.Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Marchi 3, 2023 ameshiriki kwenye swala ya mazishi ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Ntambile, Marehemu Habibu Ali Mohamed.
Akiwa kwenye swala hiyo Rais Mwinyi alimpa mkono wa pole Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid mara baada ya swala ya Maiti katika masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Mjini Magharibi.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemedi Suleiman Abdulla naye apia alishiriki swala hiyo.