Madiwani katika Manispaa ya Singida wameiomba serikali itunge sheria itakayotoa adhabu kali kwa wanaopata fedha kwa kuuza miili yao ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Ukimwi (VVU).
Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu alisema hayo mjini Singida wakati wa kujadili taarifa ya Kamati ya kudhibiti Ukimwi iliyosomwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hassan Mkata, kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Minga, Ibrahim Murua alitaka kujua kamati hiyo imeweka mikakati gani kudhibiti vitendo vinavyochangia kuenea kwa maambukizi ya Ukimwi yakiwamo madanguro yanayodaiwa kuchangia kasi ya ongezeko la maambukizi ya VVU.