Kaburi la mtoto lafukuliwa, mwili na jeneza vyaibwa


WAKAZI wa Kitongoji cha CCM-Senta, Kijiji cha Lwamugasa wilayani Geita mkoani hapa wamekutwa na sintofahamu baada ya kaburi la mtoto aliyezikwa kukutwa limefukuliwa na watu wasiojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo, baba wa mtoto, Dismas John (35) alisema mwanawe wa miaka miwili, alifariki Februari 15 na kuzikwa Februari 16, 2023 katika malalo ya kijiji hicho.

Alisema chanzo cha kifo cha mwanawe ni baada ya kuugua kwa siku mbili mfululizo, ambapo alifariki siku ya tatu wakiwa njiani kumpeleka kwenye matibabu katika kituo cha afya kilichopo mji mdogo wa Katoro.

“Tulienda kuzika katika malalo ya kijiji na baada ya hapo, tarehe 17 (Februari), ubalozi jirani na wao walipata msiba na kwenda malaloni, baada ya kufika eneo la malaloni walikuta kaburi lile limefukuliwa.

“Mwili na jeneza vyote havimo, liko wazi, mimi nilikuwa bado nipo nyumbani walinipigia simu, nikafika maeneo ya tukio kweli nikashuhudia mwenyewe, na wale watu waliokuwa wanazika pale walishuhudia.

 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo