Bweni la shule lafungwa baada ya ripoti za ulawiti wa wanafunzi

 

Mamlaka ya Uganda imefunga sehemu ya bweni ya shule ya msingi katika eneo la kati la Mubende baada ya wavulana saba wa shule kuripotiwa kulawitiwa na mlezi wa shule hiyo.

Vyombo vya habari vya eneo hilo vinaripoti kuwa mhudumu huyo alikiri mashtaka hayo mahakamani wiki iliyopita na anasubiri hukumu.

Waziri wa Elimu ya Msingi, katika Jimbo hilo Joyce Moriku Kaducu, Jumapili alisema msongamano katika shule hiyo umetoa "hali inayowezesha " unyanyasaji wa wanafunzi.

Wanafunzi 350 wa bweni katika shule hiyo walikuwa wamelala kwenye vitanda vya sitaha katika vyumba vitano vidogo, tovuti ya Daily Monitor inaripoti.

"Ninataka ninyi [wasimamizi wa shule] kuwaambia wazazi kwamba mumekuwa mkiendesha sehemu ya bweni isiyo halali na hakuna miongozo inayofuatwa," waziri alisema alipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki.

Pia aliwalaumu maafisa wa elimu wa eneo hilo kwa kukosa kukagua shule.

Shule nchini Uganda zinahitaji leseni ya serikali ili kuendesha sehemu za bweni


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo