Askari Magereza Wanawake 18 matatani kwa Kujihusisha kimapenzi na Wafungwa

Maafisa wa polisi 18 wa idara ya magereza wamepigwa kalamu kwa tuhuma za kuzama katika mapenzi na wafungwa katika gereza moja kubwa la taifa la Uingereza.


Jarida moja la nchini humo la Daily Mail linaarifu kuwa polisi hao wa kike wamemwaga unga kufuatia ufichuzi uliowakuta na sakata ya kuingia katika mapenzi na mahabusu. 


Kwa mujibu wa ufichuzi huo, maafisa hao wa polisi wamekuwa wakifaidi mapenzi ya wafungwa wa gereza la HMP Berwyn kwa takriban miaka sita na kujihusisha na vitendo vya mapenzi nao. Mark Fairhurst ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Magereza amelaumu mfumo wa kuwaajiri maafisa hao kuwa chanzo kikuu cha tatizo hilo.


"Maafisa wanaoajiriwa hawafanyiwi mahojiano ya uso kwa uso... Yote yanafanywa kupitia mtandao wa Zoom. Wengi wanaoajiriwa hawana uzoefu tosha kukabili maisha na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa wafungwa kuwapa masharti," Fairhurst amenukuliwa na The Mirror. 


HMP Berwyn ambalo ni miongoni mwa magereza makubwa zaidi nchini Uingereza na lenywe wafungwa wa jinsia ya kiume wa kitengo cha C lina thamani ya pauni milioni 250 Daily Maily linaripoti kuwa Emily Watson, 26, Jennifer Gavan na Ayshea Gunn wote wenye umri wa miaka 27 ni miongoni mwa maafisa waliokutwa na hatia ya kuzama kwenye penzi la mahabusu. 


Gavan alikuwa kwenye mapenzi na mfungwa Alex Coxon mwenue umri wa miaka 25 na kupewa kifungo cha miezi minane gerezani mnamo Disemba mwaka jana kwa hatia hiyo. 


Gunn ambaye ni afisa mwenzake naye alikutwa akichumbiana na Khuram Razaq mwenye umri wa miaka 29 na anayetajwa kuwa mfungwa hatari.


Chanzo: TUKO.co.ke


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo