Wanaume 2 Wanaoishi Pamoja na Kubadilishana Wake Zao Kila Usiku


Wanandoa wawili wamefunguka kuhusu mpango wao usio wa kawaida ambapo kando na kuishi pamoja, wao hubadilishana wenzi wao.


New York inaripoti kuwa wanne hao wanajumuisha Alysia na Tyler Rogers na marafiki zao Sean na Taya Hartless. Inaripotiwa kuwa Alysia na Tyler tayari walikuwa wazazi wa watoto wawili wenye umri wa miaka saba na minane walipoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na marafiki zao. Mnamo 2020, wanne hao walihamia katika nyumba moja na kufikia 2021, Alysia na Taya walijifungua watoto kwa tofauti ya miezi saba lakini hakuna hata mmoja kati yao anayejua ni nani kati ya wanaume hao wawili ndiye baba halisi wa watoto hao.


Alysia alifichua kwamba kadiri muda unavyosonga, watawasaidia watoto wao kuelewa msingi wa malezi yao iwapo wataonyesha nia ya kutaka kujua. "Tulitaka kufanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba kila mtu anahisi kama mzazi sawa," Taya alisema, akiongeza kuwa hakuna haja ya kufanya uchunguzi wa jeni kwani watoto bado ni wachanga. Familia hiyo kubwa ya watu wanane, ambayo imejikusanyia wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii, kwa sasa wanaishi Lebanon na mara nyingi hushiriki video za maisha yao yasiyo ya kawaida. 


"Tulipokutana, tulikuwa tukitafuta kitu rahisi na cha kimwili, lakini sote tulipokutana tulianza kupendana," waliandika. Katika moja ya video hizo, wanaume hao walifichua kuwa hubadilisha wenza kila usiku na wana uhusiano na wanawake wao tu. Wanaelezea mpangilio wao kama wenye uaminifu na hawashiriki katika mahusiano nje ya mraba huo. "Tuna vyumba viwili vya kulala kwenye ncha tofauti za nyumba, na wanaume hubadilishana vyumba kila usiku," walisema.


Kama binadamu yeyote wa kawaida, wenzi hao walikiri kwamba walikuwa na wivu sana mwanzoni, lakini hilo lilififia baada ya kuwepo kwa uaminifu. Pia walifichua kuwa japo wana wafuasi 120,000 kwenye TikTok na 30,000 kwenye Instagram, mara nyingi hupokea shtuma kali kutoka kwa wanamtandao.


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo